Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marcus anusurika kifo katika ajali

Jf Talksport Marcus Edwards Marcus anusurika kifo katika ajali

Thu, 30 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Tottenham Marcus Edwards amenusurika baada ya kupata ajali mbaya wakati akielekea mazoezini.

Picha kadhaa zimelionyesha gari la winga huyo aina ya Range Rover likiwa limepinduka.

Polisi, zimamoto na maafisa wa afya walikuwa kati ya watoa huduma za dharura wa kwanza kufika katika eneo la tukio kaskazini mwa jiji la Lisbon.

Edwards (24) ameshikwa na mshtuko lakini ametoka bila majeraha yoyote. Dereva wa gari lingine lililohusika katika ajali hiyo pia ametoka salama.

Winga huyo alikuwa akielekea kwenye mazoezi ya mwisho na klabu yake kabla ya mechi ya Ligi ya Uropa dhidi ya Atalaya ya Italia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live