Manchester United wanaweza tena kumkosa Marcus Rashford kwa safari yao ya Ligi Kuu dhidi ya Bournemouth hii leo
Mshambuliaji huyo alikosa ushindi wa wikendi iliyopita dhidi ya Wolves kutokana na jeraha la mguu lakini amefanya mazoezi wiki nzima na alitarajiwa kuwepo kabla ya kuugua tena.
Meneja Erik ten Hag alisema: “Rashford alifanya mazoezi vizuri wiki nzima lakini leo ameripoti hajisikii vizuri, kwa hiyo ni mgonjwa. Inabidi tuone atapona vipi mchana kisha tuone kesho (leo).
United wapo nafasi ya nne katika msimamo wa EPL huku akifukuziwa kwa karibu na Liverpool ambao nao wanapambana kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.