Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marcelo na Rekodi zake Madrid

Marcelo Real.jpeg Marcelo

Sun, 1 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil anayekipiga kwenye klabu ya Real Madrid Marcelo amefanikiwa kuingia kwenye kumbukumbu za klabu hiyo ya kuwa mchezaji aliyefanikiwa kubebe mataji mengi kuliko mchezaji yeyote ndani ya klabu hiyo.

Marcelo mwenye umri wa miaka 33 amefanikiwa kushinda taji lake la 24, baada ya Madrid kuifunga Espanyol goli 4-0 na kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa La liga, na yeye akifanikwa kuingia kwenye kumbukumbu za klabu ya Real Madrid huku akifuatiwa na Francisco “Paco” Gento, mwenye makombe 23.

“Kombe ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanyika, kujitoa,” alisema Marcelo ambaye aliinama kutoa heshima kwa mashabiki huku wakilitaja jina lake. “hiki ni kitu kikubwa kwa mchezaji, kushangilia nyumbani, tena mbele ya mashabiki.”

“Tumeweza kushinda ubingwa wa ligi hii, shukrani kwa timu nzima kwa kujitoa kwao,” aliongezea Vieira da Silva .

Marcelo makombe aliyofanikiwa kushinda akiwa na Real Madrid ni, klabu bingwa ulaya 4, kombe la dunia la klabu 4, UEFA Super Cups 3, Copa del Reys 2, Spanish Super Cups 5 na La liga 6

Chanzo: www.tanzaniaweb.live