Nyota wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Marcelo Viera yuko kwenye mchakato wa kuvunja mkataba na klabu yake ya sasa Olympiacos ya nchini Uturuki.
Marcelo ambaye amedumu kwa miezi sita ya kuitumikia klabu hiyo na kucheza michezo kumi tu tayari ameshafikiria kuvunja mkataba na klabu hiyo, Ikielezwa anataka kutafuta klabu nyingine na kuachana na miamba hiyo ya soka kutoka nchini Uturuki.
Gwiji huyo ambaye amecheza klabu ya Real Madrid kwa mafanikio makubw alijiunga na klabu ya Olympiacos mwezi Septemba mwaka jana akisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo, Huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.
Taarifa kutoka nchini Uturuki zinadai klabu ya Olympiacos inatambua Marcelo amepewa ofa kubwa zaidi na klabu ambayo haijawekwa wazi, hivyo ni makubaliano ya pande zote mbili kua beki huyo avunje mkataba klabuni hapo ili aelekee ambapo amepata ofa kubwa zaidi.
Marcelo baada ya kuelezwa yupo katika hatua za mwisho za kuvunja mkataba wake na miamba ya soka nchini Uturuki vilabu kadhaa vimekua vikiwinda saini ya nyota huyo, Lakini klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia alipo rafiki wake mkubwa Cristiano Ronaldo imekua ikitajwa zaidi kumchukua beki huyo.