Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Marcelo, Modric Wakutwa na Maambukizi ya COVID-19

Modric 696x392 Luka Modric na Marcelo wakiwa uwanja wa mazoezi

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid wamethibitisha kuwa nahodha wao Marcelo na Luka Modric wamepimwa na kukutwa na maambukizi ya COVID-19.

Mbrazil huyo amekuwa akijikuta kwenye benchi hivi karibuni, lakini kukosekana kwa Luka itakuwa pigo kwa Los Blancos kutaonekana, haswa baada ya kiwango chake bora kwenye mechi ya Madrid derby wikendi iliyopita.

“Real Madrid C. F. inataarifu kwamba wachezaji wetu Marcelo na Luka Modric wamepimwa na kupatikana na COVID-19,” ilisomeka taarifa ya Real Madrid.

Real Madrid watawakaribisha Cadiz Jumapili, Desemba 19, kabla ya kusafiri kumenyana na Athletic Club mjini Bilbao siku chache baada ya Jumatano, Desemba 22.

Kwa hivyo inatarajiwa kwamba Marcelo na Modric hawatakuwepo kwa mechi hizi mbili baada ya kukutwa na virusi hivyo, kwa hivyo mechi ya kwanza ambayo wanaweza kurejea ni ugenini Getafe Januari 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live