Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapungufu Simba vs Yanga yafanyiwe kazi

Simba Vs Yanga Aziz Ki Debut.jpeg Mapungufu Simba vs Yanga yafanyiwe kazi

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kila mmoja ameona mapungufu amabyo yalikuwa kwenye timu zao katika mchezo wa Kariakoo Dabi. Simba na Yanga walikuwa na kazi kuonyeshana ubabe wao.

Mwisho mshindi alipatikana na yule ambaye alipoteza alifahamika. Weka kando masuala ya matokeo bado kuna mapungufu ambayo yalionekana kwenye mchezo huo.

Kuanzia kwa wachezaji namna walivyokuwa wakitimiza majukumu yao. Kufanya kosa moja kwenye mchezo mkubwa wa Kariakoo Dabi ni kitu ambacho kinapaswa kufanyiwa kazi.

Pongezi kwa wale waliotumia makosa ya wachezaji ndani ya uwanja kupata matokeo. Wale waliofanya makosa ni muda wa kufanyia kazi makosa yao kwa ajili ya mechi zinazofuata.

Ipo wazi kwamba Simba na Yanga zina kazi kwenye mechi za kimataifa katika Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo ni muhimu kufanyia kazi maboresho yao.

Zile tambo ambazo zilikuwa awali kabla ya mchezo na baada ya mchezo matokeo yalionekana. Kikubwa ni kuamini kwamba mpira hauhitaji kelele nyingi zaidi ya uwekezaji.

Wachezaji ni muda wa kuangalia upya makosa yaliyofanyika na kuwa imara kwa mechi zijazo kwa kuwa maisha ya mpira bado yanaendelea.

Mashabiki walipata muda kuona namna ushindani ulivyo na burudani kubwa ilitolewa kwa kila mmoja kusubiri kujua nani atakuwa nani.

Kwa upande wa waamuzi licha ya kazi kubwa ambayo walifanya yapo makosa yao ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi wakati ujao ili kuwa imara zaidi na zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: