Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapunda awapa neno wachezaji wazawa kuelekea AFCON

Mapunda Awapa Neno Wachezaji Wazawa Kuelekea AFCON Mapunda awapa neno wachezaji wazawa kuelekea AFCON

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golkipa wa zamani wa Simba na timu ya Taifa Tanzania, Ivo Mapunda amesema fursa zitakazopatikana kwa Tanzania kuandaa michuano ya Afcon 2027 ni pamoja na kutengeneza wigo mpana kwa wachezaji wetu pamoja na kujiuza nje.

“Tutapata nafasi ya kuonekana vizuri kwa vijana wetu, timu zetu lakini pia kutengeneza soko zaidi au kutengeneza wigo mpana zaidi kwa wachezaji wetu hasa ukilenga Zaidi kwenda kucheza nje ya nchi,"

Hii itasaidia kwa wadau watakaokuja kutafuta vipaji kwa ajili ya mpira, ni mashindano yenye faida hasa kwenye soka,”

Mapunda amesema hayo leo Jumatano Oktoba 4, 2023 wakati wa mjadala wa Mwananchi Space ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi Communications Ltd ukiwa na mada isemayo; Fursa zilizopo kwa Tanzania kuandaa fainali za Afcon 2027.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live