Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maproo wawapoteza kina Bocco Simba

Bocco Second Goal Maproo wawapoteza kina Bocco Simba

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mabao 50 ya kufunga ya Simba katika kila mabao matatu wageni wamefunga mawili na moja wazawa ambapo wamezidiana asilimia 32.

Katika mabao hayo wageni wamehusika nayo asilimia 66, wakati wazawa asilimia 34 pamoja na kwamba wao ndiyo wengi zaidi, jambo lililowaibua wataalamu wa soka kuwataka mastaa wa kikosi hicho kuwa na ushindani sawa utakaoondoa presha kwa kocha kwenye kikosi hicho ambacho kinaongoza kwa mabao Ligi Kuu.

Mwanaspoti limegundua katika mabao 50, wageni wamefunga 33 na wazawa 17, pia wageni wanaoongoza kwa asisti.

Simba ilipocheza dhidi ya Dodoma Jiji, ilishinda mabao 3-0 Uwanja wa Mkapa, Oktoba 2, lakini moja alijifunga beki wa kati Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ambalo halijajumuishwa katika mabao 50.

MAPROO NA MABAO YAO

Moses Phiri (10),Said Ntibazonkiza ‘Saido’ (5)

Pape Sakho (6), Augustine Okrah (4), Clatous Chama (3)

Henock Inonga (2), Jean Baleke (1), Dejan Georgijevic (1 na Peter Banda (1), hivyo wana mabao 33.

WAZAWA

John Bocco (9), Kibu Denis (2), Jonas Mkude (1),

Habibu Kyombo (2), Shomari Kapombe (1), Mzamiru Yassin (2), hivyo wana jumla ya mabao 17.

WAKALI WA ASISTI

Chama (12), Mohammed Ouattara (1), Sadio Kanoute(1), Kibu (2), Mkude (1), Mohamed Hussein Tshabalala (5), Okrah (1),

Phiri (3), Mzamiru (5), Gadiel Michael (2), Kapombe (3), Saido (2), Sakho (1) na Bocco (1).

Katika pasi za mabao 40 ya Simba, wageni wana 21 wakiongozwa na Chama ambaye ametoa asisti 12, huku wazawa wakiwa na 19 wakiongozwa na Tshabalala na Mzamiru wenye tano kila mmoja.

MITAZAMO

Straika wa zamani wa timu hiyo, Zamoyoni Mogella alisema kitendo cha wageni na wazawa kuzidiana asilimia 32, kinaonyesha kocha anavyoweza kupata presha wanapokosekana wachezaji wanaotumika mara kwa mara.

“Kama idadi ya mabao ya wageni ni 33 na wazawa 17, hapo ushindani siyo mkubwa, wazawa wanalazimika kuongeza nguvu na kujua umuhimu wao ndani ya timu,” alisema.

Mtazamo wake haukupishana na wa beki wa zamani wa Simba na Yanga, Godwin Aswile aliyesema ifikie hatua wazawa wajitambue thamani yao mbele ya wageni, akisisitiza kwamba wasikubaliane kupitwa kila kitu.

“Mfano mzuri ukimuondoa Bocco ambaye ana mwendelezo na kufunga wengine pia wanapaswa kuiga hilo, juhudi haijawahi kumfelisha mtu, kikubwa wajue wageni wanawapita wapi kisha wayafanyie kazi mapungufu yao,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti