Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapro 30 walioitwa Taifa Stars gumzo kila kona

Taifa Stars Imetotaaa Taifa Stars

Fri, 22 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maproo 30 walioitwa na kocha Adel Amrouche katika kikosi cha awali cha timu ya taifa, Taifa Stars kwa ajili ya maandalizi ya fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) wameibua gumzo.

Juzi, Amrouche aliwaita wachezaji 53, kwenye kikosi hicho, kati yao 23 wanacheza Ligi Kuu Tanzania Bara na waliosalia wanacheza nje ya nchi (maproo).

Hata hivyo, idadi hiyo itapunguzwa hadi kubaki wachezaji 27, ingawa ni 23 pekee watakaoruhusiwa kucheza fainali hizo za tatu kwa Taifa Stars, baada ya zile za 1980 na 2019 zilizofanyika Nigeria na Misri mtawalia ambazo kote Stars iliondoshwa katika hatua ya makundi.

Msimu huu, Tanzania ni kati ya mataifa 24 yatakayoshiriki fainali hizo zitakazofanyikia Ivory Coast kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwakani.

Kati ya maproo 30 walioitwa na Amrouche yumo mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Norway ‘Eliteserien’, Amahl Pellegrino anayeichezea Bodo/Glimt.

Wapya wengine kwenye kikosi hicho cha awali ni Zion Nditi (Aldershot Town) na Roberto Nditi (Forfar Athletic).

Wengine ni Ayoub Bilal (FK Gorazde), Tarryn Allarakhia (Wealdstone), Miano Danilo na Twariq Ahmed (Telford United), Mark John (Kingstone), Mohammed Ali (Boreham Wood), Adam Kasa (IFK Haninge), Said Khamis (FK Jedinstvo), Cyprian Kachwele wa Vancouver Whitecaps FC 2.

Maproo wengine walioitwa ni Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki), Saimon Msuva (JS Kabylie, Algeria), Ben Anthony Starkie (Basford United FC, England), Kokola Charles M’mombwa (Macarthur FC, Australia), Joshua Ibrahim Mwakasaba (Tusker FC, Kenya).

Akizungumzia uteuzi huo, kocha wa zamani wa Stars, Charles Boniface Mkwasa alisema kuwa na wageni 30 na wazawa 23 ni ishara tosha kwamba kuna kitu benchi la ufundi limekiona kwao.

“Kwanza tunapaswa kutambua hiki ni kikosi cha kwanza tu lazima wapungue lakini ukiangalia wachezaji wa kigeni kuna vitu vingi wanavipata nje tofauti na wazawa hivyo kama walifanyiwa tathimini ya kutosha basi naamini watatusaidia,” alisema.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Biashara United, Amani Josiah alisema kitendo cha wageni kuonekana wengi kinaonyesha benchi la ufundi la Stars litakuwa na kazi kubwa ya kuwachuja tofauti na wazawa ambao wao wamekuwa wakicheza mara kwa mara.

“Watakaoathirika zaidi tofauti ni wazawa kwa sababu wao ndio watakaofanyiwa tathimini kubwa ya huko wanakotoka,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live