Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapokezi ya Wananchi yamkosha Chama

SASACHAMA Mapokezi ya Wananchi yamkosha Chama

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama amewashukuru mashabiki na wanachama wa Yanga kwa ukaribisho wa aina yake.

Jana Yanga ilimtambulisha Chama kwa utambulisho rasmi baada ya hapo awali kumtambulisha kupitia picha za kusaini mkataba. Chama amesema amefurahia na vile Wananchi walivyompokea na kuwaahidi kuwafanyia mambo makubwa uwanjani

"Nafurahi kujiunga na timu hii kubwa zaidi Tanzania. Nawashukuru Wananchi kwa mapokezi yao kwa kweli nimepokelewa vizuri. Sitazungumza mengi kwa sasa lakini nawaahidi, watafurahi uwanjani," alisema Chama.

Baada ya usajili wake kutangazwa wiki iliyopita, Wananchi wakiongozwa Msemaji wa klabu Ali Kamwe waliandamana mitaani kufurahia usajili wake.

Kama haitoshi likafanyika tukio maalum la kula keki Makao Makuu ya Yanga, Jangwani ambapo keki 17 zililiwa na Wananchi ikiwa ishara ya kumkaribisha Chama nayependelea kuvaa jezi namba 17.

Chama tayari ameungana na kikosi cha Yanga kilichoanza maandalizi ya pre-season. Yanga inatarajiwa kuelekea Afrika Kusini wiki ijayo kwa ajili ya maandalizi ya Toyota Cup ambapo Julai 28 watachuana na Kaizer Chiefs.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live