Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapipa ya Al Ahly wala sio jambo la kushangaza

Ahly Mapipa Mapipa ya Al Ahly wala sio jambo la kushangaza

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Sioni ajabu yoyote kwa kitendo cha Klabu ya Al Ahly ya Misri kuleta mapipa yao hapa nchini walipokuja kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Simba katika mashindano ya African Football League.

Ajabu nililoliona ni namna tukio kuonekana kama la kushangaza na la kipekee kiasi cha kuteka hisia za baadhi ya vyombo vya habari hasa vile vinavyorusha maudhui mtandaoni.

Nadhani badala ya kushangaa, tulipaswa kutumia jambo hilo kutoa fundisho kwa timu zetu kuwa zinapaswa kuhakikisha zinakuwa na uwekezaji mkubwa ili ziweze kufanya mambo kama hayo zinaposhiriki mashindano ya kimataifa.

Kwamba kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ni zaidi ya kucheza uwanjani na badala yake unapaswa kushinda changamoto nyingi za nje ya uwanja baada ya kufanya tathmini ya wapinzani unaokutana nao.

Hali ya hewa ina nafasi kubwa ya kuathiri ufanisi wa wachezaji uwanjani hivyo timu inapokwenda katika nchi fulani inapaswa kuandaa vifaa ambavyo vitawezesha kukabiliana na mazingira ambayo itakutana nayo.

Katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar mwaka jana, Argentina ilisafirisha shehena kubwa ya nyama na majiko kutoka kwao na kupeleka huko ambako mashindano hayo yalikuwa yanafanyika ili tu wasiathiri wachezaji na vyakula vya Qatar.

Timu ya Taifa ya England yenyewe ilisafirisha viyoyozi maalumu na kuvifunga katika kambi yao huko Qatar ili wachezaji wasiathirike na hali ya hewa ya joto ambayo imekuwepo katika nyakati za mchana kwa nchi za jangwani hasa zile za Mashariki ya kati.

Kwa hiyo ningeshauri mjadala usiwe unasifia tu mapipa na hivyo vitu vilivyoletwa na Al Ahly bali ujikite katika kuonyesha umuhimu wa vifaa hivyo. Al Ahly imetangulia inatakiwa tujifunze kutoka kwao.

Chanzo: Mwanaspoti