Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapinduzi FC yatwaa ubingwa RCL 2023

Mabingwa RCL Mapinduzi FC yatwaa ubingwa RCL 2023

Fri, 5 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kikosi cha timu ya soka ya Mapinduzi kutoka Mwanza kimeibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Kiluvya na kuwafanya waweze kuwa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wa mikoa msimu wa 2023.

Mchezo huo uliochezwa May 04,2023 majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wa soka wa Ushirika, Moshi, ambapo timu zote zilicheza kwa nguvu na kasi ya kutaka kupata ushindi mapema na hatimaye Mapinduzi Kushinda mchezo huo.

Ushindi huo ulipatikana kwa mbinde baada ya dakika 90 kumalizika na kuongezwa dakika 30 ambapo timu hiyo ilijipatia mabao 3-0 huku timu ya Kiluvya ikishindwa kuona lango la wapinzani wake.

Akizungumza na Mwanaspoti kocha wa Mapinduzi,Gilbert Daddy amesema ulikuwa mchezo mgumu sana kutokana na wapinzani wao kujipanga kikamilifu kukabiliana nao ndio mana mchezo ulienda mpaka dakika 30 za nyongeza.

"Ulikuwa ni mchezo mgumu kutokana na Hali walipokuwa nayo wapinzani wetu pia walitengeneza mbinu iliyoweza kutuzuia hasa katika kipindi Cha kwanza, hatukuweza kufanikiwa na hata tuliporudi kipindi Cha pili " alisema Gilbert.

Aidha Gilbert ameongeza kwa kusema waliazimia Kushinda mchezo huo mapema kipindi Cha kwanza lakini hawakuweza kufanikiwa hatimaye waliweza kufanikiwa dakika za nyongeza baada ya wachezaji wa timu ya Kiluvya kuchoka na kuishiwa pumzi.

"Tulitaka tumalize mchezo kipindi Cha kwanza ila hatukuweza kufanikiwa lakini wenzetu walipungukiwa nguvu katika dakika za nyongeza ndipo tukaweza kutumia udhaifu wao kupata ushindi" alisema Gilbert.

Hata hivyo timu za Mapinduzi,Kiluvya na Nyumbu zimepanda daraja moja kwa moja na zitacheza Ligi daraja la pili (first league) msimu ujao huku timu ya Tanesco ya Kilimanjaro ikipata nafasi hiyo ambapo viongozi wa soka Mkoani hapa walisema watatolea ufafanuzi badae.

Chanzo: Mwanaspoti