Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapinduzi FC uso kwa uso na Azam, Dodoma Jiji

Mapinduzi FC Mapinduzi FC uso kwa uso na Azam, Dodoma Jiji

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa mkoa wa Mwanza, Mapinduzi FC imesonga mbele katika michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa kutinga hatua ya 16 bora.

Mapinduzi imetinga hatua hiyo baada ya kuitupa nje Polisi Katavi kwa penalti 4-3 katika mchezo wa hatua ya 32 bora kufuatia suluhu (0-0) baada ya dakika 90 kumalizika.

Mchezo huo umepigwa leo Alhamisi saa 10 jioni katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, huku wageni hao wakiwakazia Mapinduzi FC na kuwalazimisha kwenda hatua ya matuta.

Huo ni ushindi wa pili kwa njia ya matuta wa Mapinduzi FC, ambayo hatua iliyopita pia waliitoa Mbao FC kwa mikwaju ya penalti katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Kufuatia ushindi huo, Mapinduzi FC itacheza dhidi ya Azam FC au Dodoma Jiji kwenye 16 bora ya michuano hiyo, ambapo Azam na Dodoma Jiji zitavaana kesho Ijumaa katika Uwanja wa Chamazi huku mshindi akiialika Mapinduzi FC hatua inayofuata.

Mapinduzi FC ni mabingwa wa Ligi daraja la tatu mkoa wa Mwanza kwa misimu miwili mfululizo ambapo msimu huu waliichapa Warriors FC ya Ukerewe mabao 2-1 katika mchezo wa fainali na wanajiandaa na Ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL) ambayo inasubiriwa kupangiwa tarehe.

Baada ya matokeo hayo, Kocha wa timu hiyo, Mussa Magogo amesema vijana wake hawakucheza vizuri na Kutengeneza nafasi za wazi lakini jambo muhimu na kusonga mbele hivyo watafanya maandalizi ya kutosha kuwakabili wapinzani wao wajao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live