Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapinduzi Balama aitabiri Dabi ya Kariakoo

Mapinduzi Balama Kipenseli.jpeg Mapinduzi Balama

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Mashujaa, Balama Mapinduzi alisema anaikumbuka dabi ya 2019, Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya Simba mbele ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli.

“Nakumbuka bao alifunga Bernard Morrison, ulikuwa mchezo wangu wa kwanza, hivyo nikawa nipo na hofu kubwa, ila nilijengwa na mastaa wazoefu, kuuona wa kawaida, maana Simba ilikuwa na kina Luis Miqussone, Clatous Chama, Meddie Kagere, kilikuwa kikosi cha moto,” alisema na kuongeza;

“Dabi ya leo naiona itakuwa ya sare ya mabao 2-2, mechi itaamuliwa na viungo, maana timu nzuri inakuwa na viungo wazuri, mfano Yanga kuna Khalid Aucho na Simba kuna Fabrice Ngoma.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live