Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapema tu! Yanga wamaliza kazi kwa Mkapa

Simba Yanga Kim Mapema tu! Yanga wamaliza kazi kwa Mkapa

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la Ufundi la Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, limeweka wazi kuwa, mpango wao mkubwa ni kupata matokeo mazuri mapema ili kuongeza hali ya kujiamini.

Yanga wanatarajiwa kuwakaribisha Simba wanaonolewa na Juma Mgunda katika Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Cedric Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga, amesema wapo tayari kusaka ushindi kwenye kila mchezo na nia yao kubwa ni kupata ushindi wa mapema.

“Kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza kikubwa tunahitaji kupata mabao mapema, hiyo itatufanya tuongeze hali ya kujiamini na wachezaji kutimiza majukumu yao kwa umakini.

“Muhimu ni kuwaheshimu wapinzani wetu na tunajua kila mchezo ni mgumu, hivyo ambacho tunalifanyia kazi mazoezini kujiandaa vizuri ili kupata ushindi,” alisema Kaze.

Rekodi zinaonesha kwamba, msimu huu katika Ligi Kuu Bara, Yanga ikiwa imeshuka dimbani mara tano, imefunga mabao manne kipindi cha kwanza kati ya mabao 11 iliyonayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live