Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapacha waliozaliwa na wazazi tofauti

Brittany Na Briana Sac Mapacha waliozaliwa na wazazi tofauti

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Brittany na Briana ni mapacha waliokuwa na ndoto moja kwenye maisha yao ya kuolewa na wanaume ambao pia watakuwa ni mapacha kama wao. Walipendana sana na kufanya Kila kitu pamoja, Kusoma pamoja shule ya Sheria na hata kufanya kazi pamoja.

Katika Tamasha la Siku ya Mapacha mwaka 2017 huko Twinsburg, Ohio, Brittany na Briana walifanikiwa kukutana na wanaume ambao walivutiwa nao Josh na Jeremy Salyers.

Mwaka mmoja baadae 2018 kwenye Tamasha lile lile la siku ya mapacha huko Ohio walifanikiwa kuvishana Pete ya uchumba, Haikuchukua muda baadae wakaamuwa kufunga pingu za maisha.

Hata baada ya harusi yao waliamuwa kuishi pamoja wote wanne kwenye nyumba moja, Miaka miwili baada ya wanandoa hao kuoana, dada hao walitangaza kwamba wote walikuwa wanatarajia kupata watoto.

Jeremy na Briana walimkaribisha mtoto wao Jax mnamo Januari 2021, huku Josh na Brittany wakimkaribisha Jett mnamo Aprili mwaka huo huo. Watoto wao wanachukuliwa kuwa ni zaidi ya ndugu (cousin) na vinasaba inawatambua kama ni mapacha wa Quaternary.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live