Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manyika amfuata Maxime Ihefu FC

Peter Manyika Ihefu.jpeg Manyika amfuata Maxime Ihefu FC

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Singida Fountain, Peter Manyika Sr, amejiunga na Ihefu FC ili kuliongezea nguvu benchi la ufundi linalooongozwa na kocha mkuu, Mecky Maxime.

Hii ni mara ya pili kwa Manyika kujiunga na Ihefu, kwani kabla ya kuajiriwa na Singida alikuwa katika timu hiyo na Mkurugenzi wa Utawala wa klabu hiyo, Muhibu Kanu alisema tayari kipa huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyewika Yanga na Mtibwa Sugar, amejiunga kambini jijini Arusha.

“Timu ipo Arusha, Manyika kajiunga tangu jana (juzi) Jumatano na anaendelea na majukumu yake kama kawaida akisaidiana na kocha mkuu Maxime,” alisema Kanu na kuongeza;

“Sababu ya timu kuweka kambi Arusha ni kutokana na upatikanaji wa viwanja vingi vya kufanyia mazoezi pia timu zipo nyingi za kucheza nazo mechi za kirafiki na yote hayo tunazingatia mahitaji ya kocha Mexime, anachotuambia tunakitekeleza kama viongozi.”

Alipoulizwa vipi kuhusu Nizar Khalfan alisema: “Mambo bado hayajakamilika, kila kitu kikiwa tayari tutawajulisha kama ilivyo kwa Manyika.”

Chanzo: Mwanaspoti