Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula na bahati mbaya kwenye Dabi

Aishi Manula Back.jpeg Manula na bahati mbaya kwenye Dabi

Wed, 8 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa namba moja wa Kikosi cha Simba, Aishi Manula karejea uwanjani na kuanza kikosi cha kwanza baada ya kuyeyuka dakika 540 ndani ya ligi.

Ikumbukwe kwamba Manula alikuwa nje kwa muda akipambania afya yake alipopata maumivu msimu wa 2022/23 mwisho kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Ihefu alipopata maumivu ya nyonga.

Mwanzo wa msimu wa 2023/24 hali yake ilielezwa kuwa ametengamaa tayari kwa mechi za ushindani lakini hakupata nafasi ya kuanza kwenye mechi sita ambazo Simba ilicheza katika ligi kutokana na kutokuwa fiti.

Ilikuwa ni siku mbaya kazi kwake kwa kuwa kwenye mchezo huo wa Novemba 5 2023 alitunguliwa mabao matano. Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live