Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula arejea Simba, Dodoma Jiji kazi wanayo

Manulaaaaa Manula

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UONGOZI wa Simba SC, umefunguka na kuwatoa hofu mashabiki wake na kuelezea kurejea kikosini kwa kipa wao namba moja, Aishi Manula ambaye hakuwepo kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United ambapo Simba ilipata ushindi wa mabao 3-0

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amefunguka kuwa: “Manula amesharejea kikosini na kuanza mazoezi na wenzake, kwa hiyo ni jukumu la kocha kumtumia au la katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.

Manula alikosekana kwa kuwa na matatizo ya kifamilia, lakini sasa amerejea na anatarajiwa leo Jumatatu kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live