Kipa tegemeo wa Simba na Taifa Stars, Shomary Kapombe ametwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka 2022 zilizotolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), huku nyota wa riadha, Alphonce Simbu akibeba tuzo ya Mwanamichezo Bora wa jumla wa tuzo hizo zilizotolewa juzi usiku Jijini Dar.
Simbu aliyeibuka pia mshindi kwa upande wa riadha nchini, aliweka heshima mwaka jana kwa kutwaa medali ya fedha katika Michezo ya Madola iliyofanyika Birmingham, England na kwenye tuzo ya jumla za juzi aliwashinda Yusuph Changarawe, Kassim Mbutike ambao ni mabondia wa ngumi za ridhaa na bondia nyota wa ngumi za kulipwa, Ibrahim Mgandera 'Ibrahim Class'.
Mgeni rasmi katika tuzo hizo zilizofanyika ukumbi wa Mlimani City, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pindi Chana alimkabidhi Simbu tuzo hizo zilizoandaliwa na BMT chini ya uratibu wa kampuni ya Radian na kudhaminiwa na Azam Media Limited, taasisi ya kifedha ya Faidika na NBC. Katika usiku wa tuzo hizo, Rais Samia pia alipewa tuzo ya heshima ya kuchangia na kutia hamasa kuwa katika maendeleo ya michezo. Tuzo hiyoalipokea Waziri Chana kwa niaba yake.
Akizungumza mara baada ya kushinda tuzo hizo, Simbu alisema amepata faraja kubwa na ushindi huo umemuongezea ari ya kufanya vyema katika mashinadano ya kimataifa ikiwa pamoja na Olimpiki ya mwakani mjini Paris, Ufaransa.
“Nimefarijika sana kwa ushindi huu na umenipa hamasa ya kufanya vyema zaidi. Naipongeza serikali kwa kuandaa tuzo hizo na pongezi za dhati kwa Rais Samia Suluhu kwa kuweka hamasa kubwa katika michezo,” alisema Simbu. Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga alisema tuzo hizo zitakuwa zinafanyika kila mwaka huku kukiwa na uboreshaji mkubwa kwa lengo la kuleta hamasa nchini hasa kwa wanamichezo chipukizi, huku Katibu Mkuu wa BMT, Neema Msitha alipongeza wadau wote kwa kufanikisha tuzo hizo na kuwaomba kuwaendelea kuwaunga mkoni.
Washindi wengine Rehema Saidi alishinda tuzo mbili, ya kwanza ya mwanamichezo bora wa mwaka kwa upande wa tenisi kwa wenye ulemavu (Wheel Chair) na tuzo ya mwanamichezo bora wa kike kwa upande wa watu wenye ulemavu.
Halfani Kianga: Mchezaji Bora wa kiume na Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Soka la wenye ulemavu. Tembo Warriors: Timu bora ya mwaka kwa upande wa wanaume soka la wenye ulemavu Kabaddi: Timu bora ya Kabaddi ya taifa wa wanawake Kabaddi: Timu bora ya Kabaddi ya taifa wa wanaume Gofu: Timu bora kwa mchezo huo ni timu ya Taifa ya wanawake Serengeti Girls Soka Wanawake: Timu Bora ni Simba Queens Gofu: Mchezaji bora wa wanawake: Madina Idd Kriketi: Timu bora ya wanawake ya chini ya miaka 19 Kriketi Wanawake: Fatuma Kibaso Kriketi Wanaume: Evan Ismail Ngumi Ridhaa: Yusuph Changalawe Ngumi za Kulipwa: Ibrahim Class Riadha Wanawake: Failuna Matanga Riadha Wanaume: Alphonce Simbu Soka Wanaume: Aishi Manula Soka Wanawake: Clara Luvanga Michezo ya Shule Wanaume: Raphael Sanga Michezo ya Shule Wanawake: Regina Serikali Kuogelea: Timu ya Taifa ya The Tanzanite Soka Wanawake: Serengeti Girls Kabaddi: Mchezaji bora wa kike: Amina Ally Mchezaji bora wa kiume: Juma Sultan Kuogelea: Mchezaji bora wa kike: Sophia Latiff Kuoegelea: Mchezaji bora wa kiume: Collins Saliboko