Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula, Okrah warejea kuivaa Ihefu

Manula Arejea Aishi Manula alikosekana chezo uliopita

Sat, 12 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Simba, Aishi Manula na Augustine Okrah wamerejea kwenye kikosi cha kwanza kinachoikabili Ihefu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji hao walikosekana katika mchezo uliopita na Singida Big Star uliomalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Kikosi kamili cha Simba kinachoanza ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Joash Onyango, Henock Inonga, Sadio Kanoute, Pape Sakho, Mzamiru Yassin, Habib Kyombo, Moses Phiri na Augustine Okrah.

Wachezaji wa akiba ni, Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Mohamed Quattara, Victor Akpan, Nassoro Kapama na Kibu Denis.

Kikosi cha Ihefu kilichoanza ni James Ssetuba, Nico Wadada, Hassan Mwasapili, Lenny Kissu, Said Ally, Samwel Onditi, Never Tigere, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Peter Mwalyanzi na Joseph Mahundi.

Wachezaji wa akiba ni, Fikirini Bakari, Mwaita Gereza, Wema Sadock, Ally Ally, John Kitenga, Mwan Thobias na Shaban Shaban.

Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ilikuwa Disemba 30, 2020 ambapo Simba ilishinda mabao 4-0, yaliyofungwa na Meddie Kagere aliyetupia mawili, Mohamed Hussein 'Tshabalala' na Chris Mugalu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live