Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manula, Fei Toto waitwa Taifa Stars, Kapombe, Tshabalala watemwa tena

TAIFA STARS SHANGWE 1 1140x640 Manula, Fei Toto waitwa Taifa Stars, Kapombe, Tshabalala watemwa tena

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kimeachiwa leo Novemba 6 ambacho kitaingia kambini kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger na Morocco.

Katika kikosi hicho kiungo wa Azam, Feisal Salum 'Fei Toto' amerejeshwa baada ya kukosekana kwa muda huku pia golikipa wa Simba, Aishi Manula naye akiitwa baada ya kupona majeraha yake yaliyomuweka nje kwa muda mrefu.

Mabeki wa Simba Mohammed Hussein 'Tshabalala' na Shomari Kapombe bado hawajawa chaguo la kocha Adel Amrouche katika kikosi chake.

Mechi ya kwanza Stars itacheza dhidi ya Niger Novemba 18 kisha na Morocco Novemba 21.

MAGOLIKIPA - Beno Kakolanya (Singida BS), Aishi Manula (Simba SC), Aboutwalb Mshery (Young Africans), Kwesi Kawawa (Karlslunden, Sweden), Metacha Mnata (Young Africans).

MABEKI - Dickson Job (Young Africans), Bakari Mwamnyeto (Young Africans), Ibrahim Hamad (Young Africans), Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Nickson Kibabage (Young Africans), Haji Mnoga (Aldershot Town, Uingereza), Abdi Banda (Richards Bay, Afrika Kusini), Edward Manyama (Azam FC), Novatus Miroshi (Shakhtar Donetsk, Ukraine), Edwin Balua (Tanzania Prisons), Abdulmalik Zakaria (Namungo FC), Omary Mvungi (FC Nantes, Ufaransa).

VIUNGO - Ibrahim Joshua (Tusker FC, Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Sospeter Bajana (Azam FC), Baraka Majogoro (Chippa United, Afrika Kusini), Feisal Salum (Azam FC), Mudathir Yahya (Young Africans), Morice Abraham (FK Spartak, Serbia), Himid Mao (Tala'ea El Gaish, Misr'), Ladaki Chasambi (Mtibwa Sugar).

WASHAMBULIAJI - Mbwana Samatta (PACK FC, Ugiriki), Saimon Msuva (JS Kabylie, Algeria), John Bocco (Simba SC), Kibu Denis (Simba SC), Abdul Suleiman (Azam FC), Ben Starkie (Basford United, Uingereza), Matteo Anthony (Mtibwa Sugar), Charles M'mombwa (Macarthur, Australia), Clement Mzize (Young Africans).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live