Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mangungu aomba radhi Simba

Mangungu Murtaza 1 1140x640 Murtaza Mangungu

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amewaomba radhi mashabiki waliokata tiketi na kushindwa kuingia uwanjani kuhudhuria tamasha la Simba Day kutokana na milango ya uwanja kufungwa mapema.

Tamasha hilo lilifanyika Agosti 6, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam likishuhudiwa na mamilioni ya mashabiki wa klabu hiyo wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Mashabiki wengi walionekana kulalamikia mfumo wa tiketi baada ya kukata tiketi zaidi ya siku tatu nyuma lakini walipofika getini walizuiliwa kuingia uwanjani kwa kile kilichodaiwa kuwa tiketi zao hazitambuliki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live