Wakati kampeni za wagombea wa uongozi nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa Simba zikifunguliwa leo Jumatatu, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Murtaza Magungu hajafika kwa kile kilichoelezwa kuwa yupo safarini.
Mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, aliyekuwa anaongoza mkutano huo wa ufunguzi wa kampeni hizo, Hassan Dalali amewaambia wajumbe kwamba Magungu alikuwa na timu Dubai na yupo njiani kurejea Dar es Salaam.
"Magungu alisafiri na timu na yupo njiani akifanikiwa kuwahi tutaungana naye na atanadi hoja zake mtasikiliza na mtaamua wenyewe kama atawafa au la.
Ameongeza "Siyo Magungu pekee aliyetoa udhuru pia kuna Asha Baraka, Seleman Haroub , Issa Masoud, Idd Kitete na Edson."
Dalali amesema waliopata udhuru watakutana na wanachama kwenye matawi yao; "Watakuja huko kwenye matawi yenu, watajieleza mtawasikiliza hii siyo kwa Dar es Salaam bali mikoa yote ya Tanzania."
Mangungu ambaye alikuwa Dubai ambako timu iliweka Kambi yake anatetea nafasi yake ambapo anachuana na Wakili Moses Kaluwa ambaye ameanza kunadi sela zake kwa wanachama.