Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mangungu: Wachezaji wapo chini ya uangalizi

Simba Training Period Simba inatazama wachezaji wake kwa karibu sana

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC bado kipo chini ya uangalizi wa madaktari pamoja na wataalamu wa afya, kufuatia ugonjwa wa Mafua Makali uliowakumba wakiwa mjini Kagera.

Simba SC ilishindwa kucheza mchezo wake wa Mzunguuko wa tisa wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sukari Jumamosi (Desemba 18) mjini Bukoba, baada ya kuthibitika asilimia kubwa ya wachezaji wake walikua wagonjwa.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC Multaza Mangungu amesema wachezaji wa timu hiyo wanaendelea vizuri, lakini bado wapo kwenye uangalizi hadi hapo watakaporejea kwenye hali yao ya kawaida.

Amesema wachezaji wao wanaendelea na mazoezi kwa sababu haiwezekani wakakaa bila kucheza, labda benchi la ufundi tu ambalo nalo pia lilikumbwa na changamoto hiyo.

“Wachezaji wetu wanaendelea vizuri kwa sasa, lakini bado wapo kwenye uangalizi wa madaktari wa wataalamu wa afya hadi pale watakaporudi kwenye hali zao za kawaida,”

“Huu ni ugonjwa, nashangaa watu wanaongea vitu wasivyovielewa, kwa hali yoyote haiwezekani Simba ambayo inatoka Dar es Salaam, Tanzania kwenda kucheza na Misri, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na timu kubwa kama Al Ahly na zingine, wakati mwingine inashinda nje ya nchi, leo hii iogope kwenda kucheza na Kagera Sugar au Tabora na KMC?” Amehoji Mangungu.

Keshokutwa Ijumaa (Desemba 24) Simba SC inatarajiwa kucheza mchezo wa Mzunguuko wa Kumi wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC mjini Tabora katika Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live