Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mangungu: Tupo tayari kukosolewa lakini.....

Mangungu Try Again(1) Mangungu: Tupo tayari kukosolewa lakini.....

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amesema uongozi wao uko tayari kukosolewa na wanachama wao na mashabiki lakini itumike njia sahihi kwa kufanya hivyo.

Mangungu ameyasema hayo kwenye hotuba yake ndani ya mkutano mkuu wa klabu hiyo na wapo baadhi ya wanachama wenzao wamekuwa hawatumii njia sahihi ya kuwakosoa viongozi wa klabu.

Mwenyekiti huyo amesema mbali na wanachama hao wachache wapo wengine wamekuwa na mfano mzuri wa kuwakosoa kwa staha na kuzingatia masilahi ya klabu yao.

"Sisi ni viongozi na binadamu, hatujakamilika tupo tayari kukosolewa lakini tutakubali kukosolewa kwa staha na sio kwa kutolewa lugha chafu, ukija vibaya tukashindwa kuvumilia tutakurudisha kama ulivyokuja," amesema Mangungu.

"Wapo wengine ambao wamekuwa wakitumia njia sahihi kutukosoa na wanakuja hata na ushauri tutachukua kwa masilahi ya klabu yetu.

"Sisi viongozi hatuwezi kujua kila kitu kwa kuwa tunajenga nyumba moja, pia tunawajibu wa kuwasikiliza wanachama na mashabiki wetu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live