Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mangungu: Hawa kina Jobe, Freddy mtawapenda

Jobe A0001 Mangungu: Hawa kina Jobe, Freddy mtawapenda

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mwenyekiti wa Klabu Simba, Murtaza Mangungu amesema usajili walioufanya ni mapendekezo ya benchi la ufundi na wanatarajia makubwa kutoka kwa nyota wao wapya.

Simba imeongeza wachezaji sita katika dirisha dogo la usajili lililofungwa wiki iliyopita huku wakiacha wachezaji tisa, sita wakiwa wazawa na watatu wa kigeni.

"Ni mambo ya kawaida kwenye uchezaji anaweza akatoka nchini kwake akiwa bora lakini akashindwa kufanya vizuri ndani ya Simba japo hatuombei hilo kwani tuna matarajio makubwa;

"Mchezaji ambaye tunamchukua mara zote tunatarajia makubwa, wakati mwingine anafanikiwa wakati mwingine anakwama. Hata sisi tusio wachezaji wakati mwingine tunafanikiwa katika maisha na wakati mwingine tunakwama. Mchezaji anaweza asifanikiwe akasumbuliwa na mazingira na vyakula," alisema.

Mangungu akizungumzia wachezaji waliowaacha alisema wamewaondoa wachezaji saba kwa makubaliano huku akikiri kuwa wengine waliomba kuondoka.

"Wachezaji wa ndani tulioongeza na wa nje ni kwasababu ya kuziba nafasi za wachezaji ambao wameondoka kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi," alisema.

Wachezaji waliosajiliwa Simba ni Pa Omar Jobe, Freddy Michael, Babacar Sarr, Edwin Balua, Saleh Karabaka na Ladack Chasambi.

Na walioachwa ni Patrick Phiri, Jean Baleke, Nasoro Kapama, Jimyson Mwanuke, Shaban Chilunda, Mohamed Mussa, Feruz Telu.

Chanzo: Mwanaspoti