Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno ya Iniesta kwa Kocha Xavi

Iniesta Pic Data Maneno ya Iniesta kwa Xavi

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Barcelona, Andrés Iniesta amefunguka baada ya ujio wa Xavi Hernandez kama kocha mkuu wa timu hayo na kusema ni mtu sahihi kwasasa na anaweza kufanya makubwa.

"Bila shaka atafaa, kabisa. Sio tu kwa sababu anajua klabu, ni nyumbani kwake, lakini pia kwa sababu amejiandaa kwa hili,"

"Hilo ndilo jambo muhimu zaidi. Sio tu kuhusu kile Xavi anawakilisha, lakini pia kwa sababu yeye ni kocha mzuri sana na amejiandaa kwa changamoto hii" aliendelea na kusema

"Namtakia kila la kheri. Nina hakika mambo yatakwenda vizuri kwasababu amejiandaa  na anafurahia changamoto,"

"Natumai mazingira yanafanya kazi kwa niaba yake. Namtakia kila la heri, kwake kama mchezaji mwenza na kwa Barca kama klabu pia" alisema Iniesta.

Hivi sasa Iniesta anakipiga nchini Japani katika klabu ya Vissel Kobe.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz