Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno ya Edna Lema baada ya kusepa Biashara United

Edna Lema Mourinho Kazo Maneno ya Edna Lema baada ya kusepa Biashara United

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kukaa msimu mmoja ndani ya kikosi cha Biashara ya Mara kocha msaidizi wa kikosi hicho Edna Lema ‘Mourinho’ ametangaza kuaga.

Edna aliwashukuru makocha wenzake, wachezaji na viongozi wa timu katika muda wote aliokuwa Mara na kikosi hicho.

“Ulikuwa ni msimu mzuri kwetu na kwangu pia, tulifanya kila kilichokuwa ndani ya uwezo wetu lakini hatukuweza kufikia malengo kwa asilimia 100 yote kwa yote tunashukuru Mungu kwa kuwa yeye ni mjuzi zaidi.

“Niwashukuru uongozi wa Biashara UTD, Benchi la Ufundi likiongozwa na Aman Josia, wachezaji wote wakiongozwa na Captain Babilas Chitembe kwa wakati wote tuliokuwa pamoja tumeishi kama familia yale mazuri tuyaendeleze na kwa yale mapungufu tusamehane pia” aliandika Edna.

Edna aliongeza kuwa timu hiyo imechangia kumkuza na kumuongezea uzoefu katika kazi yake ya Ukocha.

“Niwatakie kila lenye kheri kwa msimu ujao. Ni ngumu kusema kwaherini lakini kwa kuwa maisha ya mpira ni mzunguko tutakutana wakati mwingine. Asanteni sana Mungu awabariki,” aliongeza.

Timu hiyo imekosa nafasi ya kupanda Ligi Kuu baada ya kufungwa mabao 2-1 katika Play Off na timu ya Tabora United kwa michezo miwili ya nyumbani na ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live