Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maneno ya Diarra kwa Matampi kuhusu kipa bora, afunguka kutua Msimbazi

Matampi X Diarra X Lakred Maneno ya Diarra kwa Matampi kuhusu kipa bora, afunguka kutua Msimbazi

Sat, 18 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Yanga, Djigui Diarra amempongeza kipa mwenzake wa Coastal Union Mkongomani Ley Matampi kutokana na ushindani anaompa katika Ligi Kuu Bara.

Kauli ya Diarra inakuja kutokana na kushindania tuzo ya kipa bora na Matampi, ambapo hadi sasa katika Ligi Kuu Bara ndio makipa wanaoonekana kujiweka kwenye nafasi nzuri wakiwa wote na 'clean sheets' 13 wakibakiza michezo mitatu ili kumaliza ligi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Matampi amesema Diarra amempongeza kutokana na anavyompa ushindani msimu huu, huku akimtabiria kufanya makubwa na kikosi cha Coastal Union kwani mara nyingi amekuwa akivutiwa na aina ya udakaji wake.

"Nimekuwa nikiongea na Diarra mara kwa mara na amekuwa akisifu uwezo ambao nimekuwa nikiuonyesha. Kwangu ni jambo kubwa linaloniongezea morali ya kupambana kwa sababu ukiangalia ni mara yangu ya kwanza kucheza hapa Tanzania," amesema.

Matampi ameongeza kuwa licha ya sifa kubwa ambazo amekuwa akizipata kutokana na uhodari wake langoni, lakini suala la kuzuia mashambulizi golini linaanzia kwa timu nzima, hivyo anawapongeza wachezaji wenzake kwani wao ndio wamekuwa chachu ya kufanya vizuri.

"Tunacheza kama timu ndio maana unaona Coastal iko hapa ilipo leo. Wengi wamekuwa wakinisifia, ila wanashindwa kutambua kwamba sisi tunapambana kwa umoja wetu tukiamini ushirikiano ni chachu ya kufikia malengo tuliyoyaweka kwa pamoja," amesema.

Kipa huyo amecheza michezo 21 ya Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa na dakika 1890, huku Diarra upande wa Yanga akicheza mechi 20 ikiwa ni dakika 1755.

Matampi aliyejiunga na Coastal msimu huu akitokea Jeunesse Sportive Groupe Bazano ya Lubumbashi, DR Congo ni kipa mwenye wasifu na uzoefu mkubwa katika soka la Afrika akiwa na medali ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika alioupata alipokuwa akichezea TP Mazembe 2017.

Medali hiyo aliipata baada ya TP Mazembe kuiondosha Supersports United ya Afrika Kusini kwenye fainali kwa jumla ya mabao 2-1. Fainali ya kwanza ilipigwa Afrika Kusini na kumalizika kwa suluhu, ambapo Matampi hakucheza lakini marudiano DR Congo alianza na kuipa ushindi wa mabao 2-1, huku akipita klabu mbalimbali kama DC Motema Pembe na Kabuscorp ya Angola.

KUMRITHI AYOUB?

Nyota huyo anahusishwa kujiunga na Simba msimu ujao kutokana na mabosi wa Msimbazi kwa sasa kutokuwa na uhakika wa kipa wa timu hiyo, Ayoub Lakred ambaye anatajwa kuwa kwenye mipango ya kujiunga na Wydad Casabalanca au Raja Athletic za kwao Morocco.

Lakred ambaye mkataba wake wa mwaka mmoja wa Simba unaisha mwisho wa msimu huu, amebainisha ofa alizonazo zinamshawishi kuondoka Simba kitu ambacho klabu hiyo inapambamana kumbakisha kutokana na kuvutiwa na namna anavyoendelea kuliweka salama lango lao kipindi ambacho Aishi Manula amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha licha ya kwamba kuna ugumu wanakutana nao.

Kilichowafanya Simba kumuwahi mapema Matampi ni namna mkataba wake na Coastal Union kuwa ukingoni kumalizika ambapo utaisha mwisho wa msimu huu ukiwa na kipengele cha kuongeza mwingine zaidi lakini kipa huyo hataki kuachana na ofa hiyo ya Simba.

Simba haitaki kuingia gharama kubwa zaidi ya kutafuta kipa wa kigeni ambaye akija atahitaji kwanza kuzoea mazingira ndiyo maana wakakimbilia kwa Matampi kutokana na kuifahamu ligi baada ya kucheza kwa msimu mmoja akiwa na Coastal Union.

Chanzo: Mwanaspoti