Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mane, Salah, Mendy nani kuibuka mbabe leo?

CAF LEO Mane, Salah, Mendy nani kuibuka mbabe leo?

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tuzo ya mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2022 upande wa wanaume na wanawake inatolewa leo usiku. Hafla ya utoaji tuzo inafanyika mjini Rabat nchini Morocco ambapo jumla ya tuzo 13 zitatolewa.

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora upande wa wanaume ni Mohamed Salah wa Misri na klabu ya Liverpool, Sadio Mane wa timu ya taifa ya Senegal na klabu ya Bayern Munich na golikipa wa Senegal na klabu ya Chelsea, Edouard Mendy.

Wanaowania kwa wanawake ni Ajara Nchout Njoya wa Cameroon na klabu ya Inter Milan, Asisat Oshoala wa Nigeria na klabu ya Barcelona, Grace Chanda wa Zambia na klabu ya BIIK Kazygurt. Tuzo hizi kwa mwaka 2022 zinatolewa kwa mara ya kwanza tangu 2019, mwaka 2020 na 21 hazikufanyika kutokana na changamoto ya ugonjwa wa Uviko 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live