Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mandinga kali mastaa Man United magari yao usipime

Fdyftf3 Mandinga kali mastaa Man United magari yao usipime

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Moja kati ya timu ambazo maegesho yake ya magari yana ndinga kali na zenye thamani kubwa pale England ni Manchester United.

Mastaa wengi wa timu hii wamekuwa wakilipwa kiasi kikubwa cha pesa hali inayoonekana kuwawezesha kununua magari makubwa ya aina hiyo.

Hii hapa ni orodha ya mastaa wote wanaomiliki magari ya bei kubwa Old Trafford.

MARCUS RASHFORD - MCLAREN 765LT

Inawezekana akawa ndio mchezaji anayependa magari zaidi kwenye kikosi cha Man United. Gari ya kwanza kumiliki ilikuwa ni Rolls-Royce aina ya Black Badge Cullinan inayouzwa Pauni 390,000 (Sh1.3 bilioni) na Rolls-Royce Black Badge Wraith yenye thamani ya Pauni 700,000 (Sh2.3 bilioni) ambayo aliyauza mwaka jana.

Aliingia kwenye rekodi ya kuwa mmoja kati ya mastaa wa EPL wanaomiliki gari aina ya Lamborghini Urus na kwa sasa anaonekana sana kuendesha McLaren 765 Longtail inayouzwa Pauni 280,000.

ANTONY - LAMBORGHINI AVENTADOR

Katika sherehe za kuitwa timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia mwaka 2022, Antony alinunua ndinga aina ya Lamborghini Aventador yenye thamani ya Pauni 337,000 (Sh1.1 bilioni).

Kabla ya gari hili, winga huyu wa zamani wa Ajax alikuwa akiendesha BMW X6 yenye thamani ya Pauni 73,000 (Sh235 milioni) ambayo aliwahi kupata nayo ajali. Hata hiyo Aventador aliwahi kapata ajali akiwa anaiendesha lakini haikuwa ajali kubwa. Gari hii ina uwezo wa kukimbia kasi ya kilomita 218 kwa saa.

HARRY MAGUIRE - RANGE ROVER SPORT

Anaendesha gari kubwa aina ya Range Rover Sport linalogharimu zaidi ya Pauni 90,000 (Sh290 milioni).

Lakini gari hii ina utofauti kwa jinsi ilivyotengenezwa, ndani yake imeongezewa mapambo ya aina mbalimbali yanayovutia ikiwa ni moja ya oda zake.

Range Rover Sport ni moja kati magari yanayomilikiwa na mastaa wengi wa Man United ikiwemo Luke Shaw.

CASEMIRO - ROLLS-ROYCE WRAITH

Anatumia Rolls-Royce Wraith ambayo aliinunua kwa Pauni 324,000 ingawa pia mara kadhaa amewahi kuonekana na Cullinan.

Gari hiyo ina uwezo wa kukimbia kilomita 250 kwa saa.

Ikiwa unataka kuinunua gari hii kwa pesa za Kitanzania inatakiwa uwe na bilioni moja ya manunuzi ambayo inaweza ikaongezeka zaidi kwenye masuala ya kodi hadi kuifikisha hapa nchini.

RAPHAEL VARANE - BENTLEY CONTINENTAL GT

Beki huyu ambaye amewahi kushinda Kombe la Dunia akiwa na Real Madrid, mara kadhaa ameonekana na gari yake aina ya Bentley Continental GT inayouzwa Pauni 183,000 (Sh591 milioni).

Kabla ya hapo alikuwa akiendesha McLaren 720S na alipokuwa Madrid alikuwa akiendesha gari mbalimbali kutoka kampuni ya Audi.

Bentley Continental GT ni moja kati ya magari ya kifahari sana ikiwa na viti visivyoumiza na kasi yake ni kilomita 210 kwa saa.

ANDRE ONANA - PORSCHE CAYENNE

Ni shabiki mkubwa wa magari aina ya Porsche Cayenne.

Ingawa ana gari nyingine za muundo wa SUV, gari yake yenye thamani kubwa zaidi ni Porsche ambayo bei yake inaanzia Pauni 70,000 (Sh226 milioni).

BRUNO FERNANDES - PORSCHE PANAMERA TURBO S

Kwenye maegesho ya magari kuna ndinga kali kama BMW X5 (Pauni 85,000) na Audi Q7 (Pauni 64,000) na hata Mini Cooper.

Gari yake ya thamani kubwa zaidi anayotamba nayo ni Porsche Panamera Turbo S, yenye thamani ya Pauni 150,000 (Sh485 milioni).

Ndinga hilo lina turbo na uwezo wa kukimbia kilomita 310 ndani ya saa moja.

ALEJANDRO GARNACHO - MERCEDES-AMG SL 43

Gari hili lina thamani ya Pauni 117,000 (Sh378 milioni). Garnacho anatajwa kuwa mmoja kati ya mastaa wanaopenda sana kuendesha magari makali.

Gari hii kutoka kampuni ya Marcedes ina uwezo wa kukimbia kilomita 170 kwa saa, mbali ya hili pia amewahi kuonekana mara kadhaa na gari nyingine aina ya GLE Coupe lenye thamani ya Pauni 70,000 na V-Class inayouzwa Pauni 66,000 (Sh213 milioni).

Chanzo: Mwanaspoti