Klabu ya Manchester United, inapanga kuongeza ofa na kujaribu kumsajili kwa mkopo nyota anayekipiga Atletico Madrid, Joao Felix. Kwa mujibu wa ripoti kiwango walichonacho Pauni 6.5 milioni bado haitoshi kumng'oa kwa mkopo Mreno huyo.
Felix, 23, anawindwa na Man United baada ya Cristiano Ronaldo kujiunga na Al Nassr, Cody Gakpo akijiunga na Liverpool kwa kitita cha Pauni 44 milioni.
Lakini sasa Man United imeanza mipango chinichini kama wanaitaka saini ya nyota huyo wa kimataifa Ureno ambaye wikiendi iliyopita alifunga bao La Liga dhidi ya Elche.
Aidha kwa mujibu wa ripoti iliyoandikwa na gazeti la Marca, mashetani wekundu wanatakiwa kuongeza zaidi ya pesa waliyokuwa nayo mkononi kama wanataka kumsajili Felix dirisha hili dogo la usajili laiki kwa mkopo.
Awali Man United ilituma kitita cha Pauni 3.5 milioni kama malipo ya uhamisho wake kwa mkopo, lakini kocha anayemnoa Felix, Diego Semione anataka kitita cha Pauni 10.5 milioni amruhusu aondoke ndani ya viunga vya klabu hiyo.
Felix yupo tayari kuondoka Atletico Mardid kwasababu hana uhusiano mzuri na Simeone kwasababu hampangi mara kwa mara jambo ambalo limempa wakati mgumu.
Hat hivyo kutokana na Kiwango hicho kikubwa cha pesa itakuwa ngumu mabosi wa Man United kutoa kwa mchezaji atakayejiunga kwa mkopo utakaodumu kwa muda wa miezi sita.
Hivi karibuni Erik ten Hag aliweka wazi hatafanya matumizi mabaya ya pesa kwenye dirisha hili dogo la usajili na ataangalia kama atapatikana mchezaji anayeuzwa kwa bein chee.
Man United imefunga mabao saba katika mechi tatu walizocheza kwenye ligi bila ya kuruhusu bao kulenga langoni, lakini imepata pigo sehemu ya kiungo baada ya Donny van de Beek kpata majeraha kwenye mechi ya ligi dhidi ya Bournemouth, wikiendi iliyopta, huku Anthony Martial akiwa hatihati.
Kwasasa Marcus Rashford ndiye mchezaji tegemeo na amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Ten Hag. fowadi huyo amefunga mechi mabao manne mfululizo akiisaidia Man United kupanda nafasi nne kwenye msimamo.