Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester United yaitajia Dortmund bei ya Sancho

Jadon Sancho Saga Jadon Sancho

Tue, 21 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United inataka walau asilimia 75 ya kiasi cha pesa ilicholipa kumnunua Jadon Sancho 2021 ikiwa timu yoyote itataka kumsajili mwisho wa msimu huu.

Sancho ambaye alinunuliwa kwa Pauni 75 milioni anadaiwa kuwa katika rada za Borussia Dortmund inayotaka kumsainisha mkataba wa kudumu baada ya ule wa mkopo kumalizika.

Hata hivyo, ili kukamilisha uhamisho wa kutua Dortmund atatakiwa kukubali kupunguza mshahara wa Pauni 275,000 kwa wiki anaoupokea.

Timu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Sancho kutokana na kiwango alichoonyesha msimu huu akiwa na Dortmund hadi akaisaidia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mujibu wa ripoti kocha wa Mashetani Wekundu, Erik Ten Hag hana mpango wa kumtumia staa huyo kwa msimu ujao na amekubali auzwe.

Tangu atue Dortmund, Januari, mwaka huu amecheza mechi 20 za michuano yote, amefunga mabao matatu na ametoa asisti tatu kikiwa ni kiwango bora zaidi kwake.

MABOSI wa RB Leipzig wamempa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja zaidi mshambuliaji Benjamin Sesko ambaye anawindwa na timu mbalimbali Ulaya ikiwamo Arsenal. Mkataba wa nyota huyo unatarajiwa kumalizika 2028. Sesko anawindwa na timu nyingi barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu ambapo amefunga mabao 18.

REAL Madrid itatakiwa kulipa Pauni 60 milioni ili kuipata saini ya kiungo wa Brighton, Alexis Mac Allister katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi Ulaya. Kiasi hicho cha pesa ni mojawapo kati ya vipengele vilivyo katika mkataba wa mchezaji huyo kwa timu yoyote inayohitaji kumsajili. Staa huyo mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika 2028.

HADI sasa Arsenal haijaanza mazungumzo na kipa wa Brentford, David Raya, 28 anayeichezea kwa mkopo ikiwa itamsainisha mkataba wa kudumu. Raya msimu huu amechukua tuzo ya kipa bora na mkataba wake na Brentford unamalizika mwakani lakini hataki kurudi na ikiwa itashindikana kusaini mkataba wa kudumu Arsenal huenda akaenda Real Sociedad.

CHELSEA haijafikia muafaka katika mazungumzo na wawakilishi wa kiungo Conor Gallagher, kwa dirisha lijalo la majira ya kiangazi na kuna uwezekano ikachukua uamuzi wa kumuuza mwisho wa msimu huu ambapo timu mbalimbali England ikiwa ni pamoja na Aston Villa na Tottenham zinahitaji huduma yake. Mkataba wa kiungo huyu unamalizika 2025.

WAWAKILISHI wa Chelsea wametua Brazil kukutana na mabosi wa Palmeiras ili kufanya mazungumzo ya kina kumsajili winga wa timu hiyo, Willian Estevao katika dirisha lijalo. Palmeiras inahitaji zaidi ya Pauni 34 milioni ili kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Brazil. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2026. Msimu huu amecheza mechi 21 za michuano yote.

WAKALA wa mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta ameripotiwa kukutana na wawakilishi wa Paris St-Germain kujadili uwezekano wa mchezaji wake kutua kwenye timu hiyo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa msimu huu amefunga mabao 19 katika mechi 39 za michuano yote.

LIVERPOOL ipo katika hatua nzuri kwenye mchakato wa kuwania saini ya kiungo wa Nice na Ufaransa, Khephren Thuram kwa ajili ya dirisha lijalo ambapo ripoti zinadai anaweza kuuzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 13 milioni. Thuram mwenye umri wa miaka 23, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 27 za michuano. Mkataba wake unamalizika 2025.

Chanzo: Mwanaspoti