Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester United yaichapa Leeds ugenini

United Wins 4 Manchester United yaichapa Leeds 4-2

Mon, 21 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Manchester United imepata ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jumapili Uwanja wa Elland Road.

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Harry Maguire dakika ya 34, Bruno Fernandes dakika ya 45, Fred dakika ya 70 na Anthony Elanga dakika ya 88 wakati ya Leeds yamefungwa na Rodrigo dakika ya 53 na Raphinha dakika ya 54.

Kwa ushindi huo, Man United inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 26 na kurejea nafasi ya nne, wakati Leeds inabaki na pointi zake 23 za mechi 24 katika nafasi ya 15.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live