Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester Derby, United au City Kushinda?

Pep X Ten Haag Manchester Derby, United au City Kushinda?

Sat, 14 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majira ya saa tisa na nusu masaa ya Afrika Mashariki, wanamichezo hasa wapenzi wa soka kichaa watakuwa karibu kufuatilia kwa ukaribu mtanange wa Manchester Dabi baina ya wenyeji Manchester United na Manchester City dimba la Old Trafford Leo Jumamosi.

Huo ni mchezo wa raundi ya pili, raundi ya kwanza iliisha kwa City kushinda bao 6-3 ambapo tangia hapo United inaonekana kuimarika kiasi chake tofauti na mechi za kwanza za kocha Erik ten Hag ambapo alipoteza kiurahisi kwa Brentford na Brighton.

United ambayo iko alama nne nyuma ya Manchester City waliopo nafasi ya pili wataifikia rekodi ya kocha Sir Alex Ferguson ya mwaka 2013 ya kushinda mechi tisa mfululizo za Ligi endapo watashinda mbele ya City ambao walipoteza mchezo wa robo fainali ya Carabao kwa Southampton katikati ya wiki.

Kocha Pep Guardiola anasema United ni moja ya timu ambazo zipo kwenye mbio za ubingwa kutokana na mwendelezo wa “fomu” ya kiwango.

Tofauti na mechi nyingi zilizopita, mechi ya awamu hii angalau inaonekana kuna usawa wa midhania kiubora, ingawa pamoja na kuwa Manchester United imepanda kwenye ubora, lakini ni wazi City msimu huu imeshuka kidogo.

Timu zote mbili zitakosa huduma ya wachezaji wa eneo la ulinzi, John Stones atakosa upande wa “The Citizens” na Diogo Dalot atakosa mechi kwa mashetani wekundu, ingawa kuna wachezaji ambao wanakosa kwa muda mrefu zaidi kama van de Beek.

Ingizo jipya la Manchester United Weghorst ambaye usajili wake ulikamilika usiku wa Ijumaa hataweza kutumika kwani bado hajasajiliwa kimfumo.

Kuhusu takwimu, tangia ujio wa Pep Guardiola United wameendelea kuwa wahanga wa vipigo kutoka kwa Manchester City. Mechi tatu zilizopita kati ya timu hizo ziliisha kwa United kufungwa. City imeshinda mechi tisa kati ya 14 ambazo alisafiri kwenda Old Trafford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live