Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester City yashtakiwa kwa ukiukwaji wa matumizi ya Fedha

Manchester City Etihad Manchester City FC

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester City imeshtakiwa Ligi kuu England kwa madai ya ukiukaji wa sheria za fedha, jambo ambalo linaweza kusababisha kukatwa pointi au hata kuondoshwa kwenye Ligi. Hii inakuja baada ya uchunguzi wa miaka minne wa Ligi Kuu ya Uingereza kuhusu fedha za klabu hiyo.

Katika taarifa ya Premier League leo Jumatatu Februari 6, 2023, Man City wanadaiwa kukiuka sheria zinazohusu utoaji wa taarifa sahihi za fedha, hasa kuhusiana na mapato ya klabu, ikiwa ni pamoja na mapato ya udhamini na gharama za uendeshaji, kati ya misimu ya 2009-10 na 2017-18, pamoja na maelezo ya malipo kwa mameneja na wachezaji wakati wa kampeni za 2009-10 na 2015-16.

Adhabu mbalimbali zinaweza kutozwa Man City iwapo watapatikana na hatia ya makosa hayo, ikiwa ni pamoja na adhabu ya pointi.

Premier League pia ilipeleka City kwenye tume huru kutokana na klabu hiyo kushindwa kufuata Kanuni za Utoaji Leseni za Klabu na Uchezaji wa Haki za Kifedha za UEFA kati ya 2013 na 2018.

Mnamo 2020, City ilipigwa marufuku ya miaka miwili kutojihusisha na soka la Ulaya lakini adhabu hiyo ilibatilishwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo kwa ukiukaji huu.

Hata hivyo Klabu hiyo ilipigwa faini ya Euro milioni 10 kwa kushindwa kutoa ushirikiano lakini ikaruhusiwa kucheza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live