Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester City wahofia Rodri kutimkia Barcelona

RODRIGO DE PP Kiungo wa Man City, Rodri

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FC Barcelona imeripotiwa wanamtaka kiungo wa Manchester City Rodri, ili kuwa mrithi wa kudumu wa Sergio Busquets ambaye muda wowote anaweza kuaga Catalunya.

Barcelona wamechukua wachezaji wachache kutoka Man City katika miaka ya hivi karibuni. Kwa mfano, kikosi chao cha sasa kinawajumuisha Eric Garcia na Ferran Torres, ambao wote waliwahi kuichezea City chini ya Pep Guardiola.

Kutokana na hadhi ya klabu hiyo, Barcelona mara nyingi hutajwa kuwa mahali pazuri pa kutua kwa wachezaji wengine ambao wanaweza kuhitaji changamoto mpya baada ya kuwakilisha timu nyingine yenye mafanikio kama City.

Kwa mujibu wa Football Insider, mchezaji anayefuata kuchukua hatua kama hiyo anaweza kuwa Rodri.

Tovuti hiyo inaeleza kuwa Barcelona wanaonyesha nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania huku wakitafuta mrithi wa muda mrefu wa Sergio Busquets kwenye safu ya kiungo.

Na kwa upande wao, viongozi wa Man City wanaamini Rodri anaweza kutaka kurejea La Liga.

Kumpoteza itakuwa pigo kubwa kwa Guardiola, kwani Rodri amecheza mechi zaidi ya 180 tangu ajiunge na City akitokea Atletico Madrid mwaka 2019.

Msimu huu, amehusika mara 31 katika mashindano yote, akianza mechi zote isipokuwa moja ya Ligi Kuu ya City hadi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live