Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester City wageukia kitasa cha Ufaransa

CA4552D7 3975 4F15 861A 4988130B614E.jpeg Mlinzi wa Ufaransa, Theo Hernandez

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester City wanamtolea macho beki wa Ufaransa na AC Milan, Theo Hernandez kwa ajili ya kumsajili dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Hernandez ambaye ana umri wa miaka 25, amekuwa mchezaji maarufu wa Les Bleus kwenye Kombe la Dunia huko Qatar na alikuwa sehemu ya timu ambayo iliiondoa England katika robo fainali hapo jana.

Na kwa mujibu wa Calciomercato, mpango unaweza kuwa unafanyika kumleta beki huyo wa kushoto Etihad siku za usoni.

Kiwango cha Hernandez kinaendana na Falsafa za Pep Guardiola, ambaye ni mtaalamu wa soka linalotegemea kumiliki mpira na kutawala mchezo. Akiwa na mchango wa mabao 49 katika mechi 140 za Milan, nyota huyo wa Serie A anaweza kuongeza ubora kwenye kikosi cha City.

Bahati yake ndani ya jezi ya Ufaransa imekuja kutokana na jeraha alilopata kaka yake Lucas, lakini beki huyo wa pembeni alitumia nafasi yake chini ya Didier Deschamps, iwapo ataendelea kucheza, anaweza kuwa katika njia ya kuisaidia nchi yake kutetea Kombe la Dunia na kuwa timu ya tatu katika historia kufanya hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live