Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manchester City Waweka Rekodi Nyingine EPL

Man City Uefa City watengeneza rekodi EPL

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baadaya ushindi wa 4-0 dhidi ya Newcastle United jana jioni Uwanja wa St. James’ Park, Newcastle.

Mabao ya Manchester City yamefungwa na Ruben Dias dakika ya tano, Joao Cancelo dakika ya 27, Riyad Mahrez dakika ya 63 na Raheem Sterling dakika ya 86 huo ukiwa ushindi wa nane mfululizo na wa 34 mwaka huu.

Kocha Pep Guardiola ameiongoza Manchester City akiweka rekodi mpya ya kushinda mechi nyingi mwaka mmoja baada ya ushindi wa jana.

Manchester City wamevunja rekodi iliyowekwa na Liverpool chini ya kocha Bob Paisley kushinda mechi 33 mwaka 1982 na wanafikisha pointi 44 katika mechi ya 18 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya Liverpool iliyocheza mechi 17.

Hali ni mbaya kwa Newcastle United kwani wanabaki na pointi zao 10 baada ya mechi 18 katika nafasi ya 19 kwenye ligi ya timu 20, ambayo mwisho wa msimu tatu zitashuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live