Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara ndiye anaujaza Uwanja Simba Day - Mchambuzi

Manara Er (14).jpeg Haji Manara akiwa Simba Day

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Alex Ngereza amedai kuwa aliyewahi kuwa Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ndiye anayeujaza Uwanja wa Mkapa kwa mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kununua tiketi katika michezo mbalimbali ambayo timu yao inakuwa inashiriki.

Ngereza amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Simba kuuza tiketi zote kuelekea Tamasha lao la Simba Day na kuweka historia ya kumaliza tiketi zote 60,0000 siku tatu kabla ya mchezo.

"Manara ndio alitengeneza hii hali ya mashabiki wa Simba kuipenda timu yao ndio maana imekuwa rahisi kuujaza uwanja tangu zamani ila sio Ahmed Ally kama ambavyo wengi wanasema.

"Wakati Manara akiwa msemaji wa Simba alifanya kila kitu kuhakikisha mashabiki wanakuwa na imani na timu yao kitu ambacho kimesababisha mpaka leo hii mashabiki wanaiamini na kuipenda timu yao hata kununua ticket imekuwa rahisi. Bila Manara Simba wasingekuwa hivi walivyo sasa hivi," amesema Alex Ngereza.

Ikumbukwe kuwa, Manara amewahi kuwa msemaji wa Simba kabla ya kugombana na uongozi wa timu hiyo na kuondoka klabuni hapo Julai 2021, kisha kuibukia kwa watani zao Yanga ambayo anaitumikia mpaka sasa.

Tamasha la Simba Day litafanyika kesho Jumapili, Agosti 6, 2023 likiambatana na sherehe, burudani na tukio la kutambuslisha wachezaji wote wa Simba msimu huu kisha mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia ambapo Mgeni rasmi atakuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Chanzo: Mwanaspoti