Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara maji yamfika shingoni, aapa kuanika ukweli hadharani

MANARA 35454657 1 Msemaji wa Yanga, Haji Sunday Manara

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya wiki iliyopita kusambaa kwa video iliyomuonesha akijibizana na Rais wa TFF, Walace Karia na baadae mtangazaji wa kituo cha E-fm Jemedari Said kuandika kuwa Mseamji huyo wa Yanga aligombana na Rais Karia na kumtolea maneno machafu.

Hatimaye Msemaji wa Yanga Haji Manara, ameahidi kuzungumza na wanahabari leo Julai 5 kuanzia saa tano asubuhi kubainisha kile ambacho kilitokea Jijini Arusha.

Haji na Karia walionekana wakijibizana katika clip ya video ambayo haikuwa na sauti katika mchezo wa Fainali ya Azam Sports Federation iliyopigwa Julai 2 katika Uwanja wa Kumbu Kumbu ya Sheikh Amri Abeid.

Kuwa karinu na Tanzaniaweb tutakuletea moja kwa moja matangazo ya mkutano huo na kujua kile kinachokwenda kuzungumzwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live