Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara kuwaburuza Simba Mahakamani

Manara 3?fit=600%2C420&ssl=1 Haji Manara, Msemaji wa Yanga

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu Yanga Haji Manara amesema anakwenda kuwashitaki waajiri wake wa zamani, Klabu ya Simba kwa kumtumikisha bila mkataba.

“Naenda Mahakamani kuwadai fidia simba wamenitumikisha bila mkataba, na nataka iwe fundisho kwa Taasisi zote zinazoajiri watu na kuwatumikisha bila mikataba. Nitaenda mahakamani kudai haki yangu, nawadai Simba pesa nyingi, wamenitumikisha miaka zaidi ya 6".

“Nimefanyiwa dhuluma, hawa sio binadamu na kwakweli mimi nina kifua sijawahi kusema ila siku nikisema mtanielewa, kisa umaarufu eti mtu ananichukia. Na iliwauma zaidi mimi kwenda Yanga, walinifanyia mambo mengi mabaya, nitadai haki yangu, nimeaanda mawakili 10,” amesema Manara.

Alipotafutwa kuzungumzia sakata hilo mwenyekiti wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema

"Ni sawa tu aende mahakamani na sisi tutasubiri wito kutoka katika mamlaka za sheria"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live