Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara kuja na PPP Yanga

Ppp Pic Data Manara kuja na PPP Yanga

Mon, 1 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSEMAJI wa klabu ya Yanga, Haji Manara amemsifu kocha wa timu hiyo, Nassredine Nabi kwa namna ambavyo timu hiyo inavyocheza soka lake la pasi nyingi.

Yanga katika mchezo wao uliopita  dhidi ya  Azam walipiga pasi 23 kuanzia kwa kipa mpaka wachezaji wa mbele na Jesus Moloko aliweka wavuni bao la pili.

Manara amesema mpaka sasa katika timu yao wachezaji wao wote wanapiga pasi na hilo lilianza kujitokeza katika mchezo wao dhidi ya KMC

“Tunacheza PPP yaani Piga pasi, Pokea na Pita mbele na hii imeanza kujitokeza katika mchezo wa Kmc lakini hata mchezo wa juzi bado tumeendelea,” amesema Manara.

Msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi amesema anamsifu kocha Nabi kwa kuitengeneza timu hiyo na sasa kucheza soka safi na la kuvutia.

“Nabi ni Profesa ameifanya Yanga kupiga pasi nyingi wakati huo huo timu ikipata ushindi, kumpongeza ni lazima kwa kazi anayoifanya.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz