Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara awashukuru TFF

Manara A0004 Manara awashukuru TFF

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu ya Yanga Sc, Haji Manara ametoa shukrani kwa wadau mbalimbali wa soka waliokuwa pamoja nae kwa kipindi chote alichokuwa akitumikia adhabu ya kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miaka miwili.

Manara ambaye amemaliza adhabu yake aliyofungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi, adhabu ya miaka miwili pamoja na faini ya milioni 10 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF, Wallace Karia, amesema licha ya kuwa nje ya ofisi lakini waajiri wake wamemuongezea mkataba na mshahara.

“Sio kila adhabu haiumi, inauma na muda mwingine unatakiwa kuvumilia. Nawashukuru sana TFF na kamati zake ambao wamefanya jambo jema na muda mwingine nilikuwa nakutana hadi na viongozi wao katika shughuli mbalimbali za kijamii

“Mtu akiomba radhi ni uungwana na sio kama umekosewa, muda mwingine tunaomba radhi kuepusha mambo. Hao wanaonichukia na kuniponda ndiyo wananisaidia na sina shida na mtu," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live