Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara awapiga dongo Yanga

Kiingilio Pic Data Manara awapiga dongo Yanga

Fri, 19 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thomas Ng'ituMore by this AuthorBy Ramadhan EliasMore by this Author MKUU wa Kitengo cha Habari Simba, Haji Manara ni kama vile ameipiga dongo Yanga baada ya kusema klabu kubwa ikiwa inawalalamikia marefa wanakosea.

Maneno ya Manara yanakuja muda mchache baada ya Uongozi wa Yanga kuzungumza na Waandishi wa Habari wakiwalalamikia waamuzi namna ambavyo wanachezesha mechi zao.

Akizingumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa, Februari 19, Manara amesema ni kitu cha kushangaza kwa timu kubwa kulalamikia waamuzi hadharani.

"Simba huko tumeshatoka hatuwezi kukaa tukianza kuwalalamikia waamuzi, yaani nyie mnakosa magoli ya wazi wenyewe halafu mnawalalamikia waamuzi, Mbeya City wafungeni tano halafu muone hao waamuzi watafanya nini," amesema Manara.

Manara ameongeza kwa kusema kuwa, "Halafu wewe kaka yangu kila siku unapelekwa kuongea mambo mabaya, mbona haupelekwi kwenye kutambulisha wachezaji inabidi ushtuke kwa kweli".

"Mdogo wako nikija hapa naongea tu mambo mazuri zuri, ukinipa mambo mabaya walaa siyataki,".

Chanzo: mwanaspoti.co.tz