"Kazi iliyofanywa na GSM kwa Yanga ni kazi kubwa ambayo haina mfano wake, Yanga ilipitia changamoto nyingi lakini tangu GSM ilipoingia kuna mabadiliko makubwa sana na ndio maana siku hizi kelele zimekuwa nyingi yaani kuna Watu walitengeneza himaya hivi kwamba 'Untouchable sisi Wakubwa sana na hivi', GSM ameziba hilo gap hususani la kifedha hakuna kelele za kudai chochote sasa hivi Yanga"
"Kuwaleta La Liga sio kitu cha mchezo Mimi najua La Liga nimewahi kuwa Balozi wa La Liga, kwahiyo GSM wanastahiki kupewa heshima yao na Wana Yanga lakini na Watu wa mpira wote, sasa wameingia kudhamini Ligi yetu hii na hizi kelele mnazosikia ni za muda tu huwezi kukataa hela yaani nakuhakikishieni ni muda tu mambo yote yatakaa vizuri
"Sote tunahitaji mpira tutashindana tutacharuana utani na nini lakini wote tunahitaji fedha za kuendesha Timu no matter what!, nawashukuru sana GSM"
"Niliona sehemu Watu wanasema Yanga wanauza Katiba, Ndugu zangu Katiba hii ya Yanga haiwezi kuwa kubwa kuliko Katiba ya Tanzania, nani aliyewahi kupata Katiba bure hapa ya Tanzania?, si zinatengenezwa hizi na zinachapishwa"
"Katiba hii kila mmoja anaijua Wanachama na Mashabiki zetu wanaisoma, Katiba gani iliyokuwa wazi ya mpira?, jiulizeni swali nyie Katiba nyingine mnaziona?, sasa hoja tena inahamishwa eti tunauza Katiba, hivi kuna Katiba inayotolewa bure?, nenda pale kwenye Ofisi za Serikali au Duka la Serikali kama utapata bure"
"Katiba ya Nchi, sisi Watanzania nenda pale waambie Mimi Mtanzania nipeni Katiba yangu bure, nenda pale uone watakavyokufanya, kutakuja Wagambo watakufanya vitu vibaya watafyetua nyonga zako zote"
"Ukiona Watu wanaficha Katiba yao ujue yaliyomo sio wanayotekeleza" Amesema Manara