Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara awahofia Simba dabi ya Kariakoo

Manara Mshs Haji Manara

Sat, 20 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara ameonesha kuwahofia wapinzani wao, Simba SC kuelekea mchezo wa leo wa watani wa jadi akidai kuwa mechi ya dabi ni ngumu na ina mambo mengi, hivyo wachezaji wasijiamini kupitiliza.

Manara amesema hayo zikiwa zimesalia saa chache kabla ya mchezo huo kupigwa leo katika Dimba la Mkapa huku Yanga wakipewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda mchezo huo.

"Haitakuwa mechi rahisi leo kama wengi tunavyoaminishana, Derby ya Yanga na Simba ni kitu kingine kabisa na ina mambo mengi zaidi ya vile tujuavyo.

"Inawezekana Yanga tunapewa nafasi kubwa ya kushinda leo, lakini nisingependa hii iingie hadi kwa wachezaji wetu, wajue kabisa over confidence ya washabiki haihusiani na uhalisia wa ndani ya pitch.

"Waende uwanjani wakijua wanaenda kukutana na wanaume wenzao, ambao wana hasira na kumbukumbu mbaya ya kufedheheshwa kwenye mechi iliyopita ya kichapo cha goli tano. Waje kikubwa na watambue tunawaamini, na InshaAllah tutashinda vizuri," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live