Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara atoa vifaa vya michezo Arumeru

97672 Pic+manara Manara atoa vifaa vya michezo Arumeru

Mon, 2 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arumeru. Afisa Habari wa Simba, Haji Manara ameonyesha ‘umwamba’ kwa kuingia katika himaya ya mtani wake DC wa Arumeru, Jerry Muro katika tukio lililofanyika Kijiji cha Kilinga Kata ya Songoro.

Manara ametokea mjini Moshi kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon hakusita kumpiga kijembe mtani wake akidai ataendelea kufika wilayani humo kuhamasisha michezo kwakua hakuna mtu anayeweza kufanya hivyo.

“Simba baba yao, nasema Simba baba yao, Simba ni mabingwa wa Tanzania hilo linajulikana kwa kila mtu hata watoto wadogo wanalijua,” alisema Manara huku akishangiliwa na mashabiki wa timu hiyo.

Akiwa ameambatana na mwenyeji wake mdau wa michezo, Joel Nasari alishiriki kugawa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh 2 milioni vilivyotolewa na Nassari kwaajili ya timu ya Kilinga Football Club (KFC).

Manara alisema maeneo ya vijijini yana nafasi kubwa kuwatoa wachezaji wazuri wanaoweza kufika mbali katika medani ya soka kutokana na mazingira yanayowazunguka na vyakula wanavyopata tofauti na wachezaji wa Dar es Salaam waliozoea chips.

“Ninyi mnaweza kufanya maajabu katika soka msijione wanyonge kwa sababu mpo kijijini, Mbwana Samatta mwenyewe tunamuona anatoka jijijini Mbagala, jambo la msingi ukitaka kufanikiwa katika soka unahitaji muda mwingi wa kupumzika na kupunguza starehe zisizo na maana,”alisema Manara

Pia Soma

Advertisement

Naye Nassari alisema michezo ni sehemu ya kuwaleta pamoja vijana ili kuibua vipaji vyao na ujio wa Manara utahamasisha vijana kuona kila kitu kinawezekana katika maisha ya soka bila kujali anakotokea mchezaji au ugumu wa kupata vifaa vya michezo.

Alisema ataendelea kushirikiana na wadau wengine wa michezo kuhakikisha timu ya KFC inakua timu kubwa na kuibua wachezaji watakaofikia kucheza ligi Kuu.

Chanzo: mwananchi.co.tz