Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara ataka 'Yanga Anthem'

Manara XGSM Day Manara ataka 'Yanga Anthem'

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka kwa El Bugatti Haji Manara; “Nyimbo rasmi ya FC Madrid, kila Madrid inapocheza popote pale Washabiki wake huimba hiyo nyimbo kabla na baada ya Mechi, huimba pia wakati mechi ikiendelea kuchezwa.

“Nguvu ya wimbo huu maarufu ni pale Madrid ikiwa inacheza nyumbani Santiago Barnabeu, Madridista wote huimba kwa nguvu sana na kuleta hamasa kubwa uwanjani.

“Ihave a dream,One Day Yanga iwe na Nyimbo yake rasmi (Club Anthems) yetu wenyewe sio ya kucopy, nyimbo itakayokuwa na maneno yatakayotutambulisha Sisi ni nani, Nyimbo itakayoiambia Dunia Sisi ndio Wananchi, Nyimbo itakayobeba ujumbe wa hamasa kwa Wachezaji na Kila mmoja uwanjani,

“Vuta picha pale kwa Mkapa Watu elfu hamsini wakiimba kwa pamoja huku wakiwa wima,feelings za Wachezaji zinakuwaje?

“Tunashinda kila kitu lakini hamasa yetu hailingani na Matokeo tuliyonayo sasa, na kwangu Club Anthem ni kitu muhimu sana kwenye hamasa, tunao wasanii wengi magwiji wa uandishi wa tungo, tuwape concept yetu, tutengeneze kitu chetu wenyew, kitaongeza hamu ya Washabiki wetu kujaa viwanjani.

“Bahati mbaya kwa sasa sina Mbawa, May be Mungu akijaalia kunipa mbawa zangu one day,hii itakuwa agenda yangu ya kwanza InshaAllah,Young Africans FC Official Club Anthem.” -Ujumbe wa Haji Manara,

Chanzo: www.tanzaniaweb.live